Mwanaharakati wa mrengo wa kulia, Charlie Kirk, auawa Utah – Global Publishers



Mwanaharakati Charlie Kirk

Mwanaharakati Charlie Kirk, mshirika wa karibu wa Rais wa Marekani Donald Trump na mwanzilishi wa Turning Point USA, ameuawa kwa kupigwa risasi katika chuo kikuu nchini Marekani. Gavana Spencer Cox ameuita tukio hilo “uuwaji wa kisiasa.”

Kirk, mwenye miaka 31, alikuwa akihutubia wanafunzi aliposhambuliwa kwa risasi moja kutoka juu ya jengo. Licha ya uwepo wa polisi na walinzi binafsi, risasi hiyo ilimjeruhi shingoni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Rais Trump alimtaja Kirk kama “shujaa wa ukweli na uhuru,” huku viongozi wa pande zote mbili wakilaani tukio hilo. Polisi bado wanamsaka mtuhumiwa mkuu.

Tukio hili limeongeza hofu ya kuongezeka kwa vurugu za kisiasa Marekani.