Ijumaa, 5 Septemba 2025 – Embu, Kenya. Ripoti mpya ya elimu imetoa wito kuchukua hatua za haraka kulingana na ushahidi wa kitafiti ili kushughulikia mapungufu yaliyopo, hayo yameangaziwa katika Mkutano wa Sita wa Education Evidence for Action (EE4A) na EDF unaofanyika kila baada ya miaka miwili kabla ya kuzinduliwa rasmi baadaye mwaka huu.
Ripoti hiyo inapendekeza tafsiri ya haraka ya taarifa zinazotokana na ushahidi ili kuingizwa katika sera za serikali kwa utekelezaji mashuleni, ili kushughulikia tatizo la Umaskini wa Kujifunza Duniani (kwa mujibu wa Benki ya Dunia na UNESCO – ni kitendo cha mtoto wa miaka 10 kutoweza kusoma na kuelewa maandishi katika umri huo).
Ripoti hii imeandaliwa na shirika la What Works Hub for Global Education (WWHGE) kwa ushirikiano na Global Education Evidence Advisory Panel (GEEAP) na British Council kama washirika wakuu.
Ripoti inabainisha kwamba:
-
Msingi wa elimu ni muhimu – bila huo, watoto huachwa nje ya fursa za baadaye za kujifunza.
-
Tunajua kinachowezekana kufanyika – mbinu shirikishi za ufundishaji, maendeleo ya kitaaluma ya walimu, na kuchukua hatua panapohitajika zinaweza kuboresha matokeo kwa kiwango kikubwa.
-
Ushirikiano huleta matokeo – kwa kujumuisha ushahidi kutoka mataifa mbalimbali na sera za ndani pamoja na mbinu za darasani, serikali na washirika wanaweza kufanikisha matokeo endelevu ya ujifunzaji.
EE4A (Education Evidence for Action) ni mkutano unaofanyika kila baada ya miaka miwili na mpango unaounganisha tafiti za elimu na maamuzi katika sekta ya elimu. Zizi Afrique Foundation imekuwa kiungo muhimu kama mwandaaji na mwenyeji wa mkutano huu wa EE4A, ambapo wadau wa elimu na watafiti hukutana kujadili masuala muhimu na kuongoza sera pamoja na utekelezaji wake.
What Works Hub for Global Education ni ushirikiano wa kimataifa unaofadhiliwa na Ofisi ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Uingereza, Jumuiya ya Madola na Ofisi ya Maendeleo pamoja na taasisi ya Gates Foundation, unaojikita katika kubaini mbinu bora za kutekeleza mageuzi ya elimu kwa kiwango kikubwa. Jukwaa hili shirikishi linahusisha washirika 12 wa kimkakati na washirika 43 wa muungano, likisimamiwa na Blavatnik School of Government kama taasisi mwenyeji wa programu.
Katika mkutano huo, WWHGE liliwakutanisha viongozi wa elimu kwenye kikao kilichojulikana “Kuimarisha Ushahidi wa Mfumo: Kutengeneza Ramani ya Mageuzi ya Elimu Nchini Kenya.” Kitivo hiko kilisisitiza dhamira yake: kuchukua ushahidi thabiti wa kimataifa, kama ilivyo kwenye Ripoti ya Elimu ya GEEAP, na kuhakikisha kwamba inaingia katika sera za serikali na hatimaye mashuleni.
Kupitia ushirikiano na wizara, taasisi za mafunzo kwa walimu, na mashirika ya ndani, WWHGE inasaidia nchi kutafsiri mapendekezo hayo kuwa mageuzi ya vitendo yanayobadilisha moja kwa moja namna walimu wanavyofundisha na wanafunzi wanavyopata maarifa ya msingi.
Mpango wa British Council – Learning and Life for Global Education (LL4GE) pia uliwasilishwa kwenye mkutano huo. LL4GE unaunganisha kusoma, lugha na stadi za maisha ili kuwapatia vijana ujuzi wa kitaaluma na kijamii, kuwaandaa kwa ajira za baadaye, ustahimilivu na uwajibikaji wa kiraia.
Kwa pamoja, WWHGE (kwa kushirikiana na GEEAP), British Council, na LL4GE wanaunda mshikamano wenye nguvu: kuchochea maendeleo ya ustadi katika kusoma kupitia mageuzi ya sera hadi darasani pamoja na kukuza maendeleo ya jumla ya wanafunzi.
What Works Hub for Global Education, kwa kushirikiana na GEEAP, British Council, na washirika wengine, sasa wataendeleza mapendekezo ya Ripoti ya Elimu kwa kuyaingiza kwenye ajenda za mageuzi ya kitaifa na kusaidia serikali kuyatekeleza mashuleni kwa kiwango kikubwa. Hii inaashiria awamu inayofuata ya dhamira ya WWHGE: kuhakikisha kila mtoto, bila kujali mazingira yake, anafaidika na mikakati iliyothibitishwa katika kupata ustadi wa msingi wa kusoma na kujifunza.
Kwame Akyeampong, Profesa wa Elimu ya Kimataifa na Maendeleo katika Chuo Kikuu Huria, Uingereza