Kwa Mkapa ‘full house’ | Mwanaspoti

Baada ya kusuasua kuingia uwanjani mashabiki wa Yanga hadi saa 10:45 Uwanja wa Mkapa ulikuwa umejaa (full house), kutokana na mafuriko ya mashabiki.

Licha ya burudani kuanza mapema uwanja ulikuwa na mapengo, lakini hadi kufikia muda huo mashabiki walikuwa wamejaa na kuendelea kuburudika na burudani.

Pamoja na uwanja kuonekana kujaa mashabiki wa Yanga wanaonekana kuendelea kuingia uwanjani tayari kushuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali sambamba na timu.

Wingi wa mashabiki waliojitokeza kwa Mkapa imekuwa shangwe kwao, kwani wamekuwa wakihanikiza shangwe kuufanya uwanja huo kuwa na kelele za hapa na pale.