Manara aibua shangwe kwa Mkapa 

KAMA kawaida ya Haji Manara awamu hii ameingia na warembo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salamaa panakpofanyika tamasha la Wiki ya Mwananchi.

Hilo ni tamasha la saba kwa Yanga tangu lilipoanzishwa 2019 chini ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msolla.

Manara amevalia nguo za kijani, ambapo baada ya mashabiki kumuona walishangilia kuonyesha wanafurahia uwepo wake.

Tangu Manara alipohamia Yanga akiwa kama msemaji na sasa mwanachama wa kawaida amekuwa akipewa nafasi ya kutambulisha wachezaji wa msimu.

Baada ya kupanda jukwaani aliposema “Wananchiiiiiiii” shangwe lilipuka kutoka jukwaani, huku mashabiki wakiwa wamewasha tochi zao za simu.

Manara ndiye anatambulisha wachezaji wa msimu wa 2025/26 unaoutarajia kuanza Septemba 17. “Tupo hapa kwa ajili ya kuitangaza wachezaji wa msimu mpya,” amesema.