Mbinu za kupeperusha mawazo ya kujiua

Kila mwaka ifikapo tarehe 10 Septemba ni Siku ya Kuzuia Kujiua Duniani. Siku hii imeadhimishwa siku mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka  huu hadi sasa kuna matukio ya kujiua zaidi ya 720,000 ambapo wanaume wanaongoza mara mbili  zaidi ya wanawake.

Vifo vitokanavyo na kujiua vinashika nafasi ya tatu duniani kwa vijana wenye umri wa miaka 15-29 ambapo zaidi ya asilimia 73 ya vifo hivyo hutokea nchi zenye kipato cha chini na kati.

Nchi tatu  zinazoongoza kwa kujiua duniani ni Greenland, Guyana na Lithuania. Afrika nchi ya Lethoto ndio inayoongoza.

Mambo yanayoweza kuchangia mawazo na tabia za kujiua ni pamoja na hali ya afya ya akili, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe, kujitenga na jamii, matatizo ya kiuchumi, ajira, elimu, mifarakano ya uhusiano na kuugua.

Mawazo ya kujiua ni wakati unapofikiria au kuhisi kushughulishwa na wazo la kifo na kujiua. Mawazo haya yanaweza kuja na kuondoka. 

Huenda ukawa na mawazo ya kujiua hadi ukapanga mpango wa kujiua.

Njia rahisi za kupeperusha mawazo ya kujiua ni hizi hapa:

Moja, kufika katika kliniki maalum za afya ya akili na kueleza tatizo lolote lililokuganda akilini. Eleza kwa uwazi jambo linalokukosesha raha kwa washauri nasaha na tiba.

Mbili, jichanganye na jamii ikiwamo watu wako wa karibu, zungumza  nao katika mambo ya kukupa burudisho na hisia chanya.

Tatu, fanya mazoezi mepesi mchanganyiko  ikiwamo ukimbiaji wa makundi kama marathon, mazoezi ya vituo vya mazoezi na ufanyaji mazoezi ya Yoga.

Nne, pale mawazo ya kujiua yanapokujia, haraka ingilia hali hiyo kwa kufanya kitu kitachofifisha wazo hilo. Mfano unaweza kuimba au kusikiliza miziki wa kuchangamka. Au soma kitabu au chezea michezo katika simu janja. 

Tamo, waza na panga mambo mapya ambayo ni rafiki, ikiwamo kujifunza ujuzi mpya wa kuvutia ikiwamo kupiga kinanda au gitaa na ubunifu mbalimbali.

Sifa, tumia huduma za usingaji au sauna, kuogelea au kuoga muda mrefu maji ya moto. Huduma hizi zinaleta utulivu wa kiakili.

Sana, epuka mazingira au vitu vinachochea kuwaza kujiua. Mfano epuka mazingira ya unywaji pombe au vilevi na dawa za kulevya.

Nane, waza mambo chanya, zingatia kutimiza malengo yako ya muda mfupi na mrefu. Fanya kazi au soma kwa juhudi na hakikisha unatimiza malengo hayo.

Ruda, jikite katika tamaduni nzuri na imani sahihi, soma vitabu vya dini na ongea na viongozi wa dini na wa kijamii.

Kumo, endapo mawazo yanakujia hasa nyakati za siku na unakosa usingizi na unasikia sauti zinazokuambia jiue, fika katika huduma za afya mapema.

Ushauri, kuzifikia huduma za afya ya akili kirahisi ni muhimu ili kuzuia kwa ufanisi tatizo la mawazo ya kujiua. Jamii iwasadie waathirika bila kuwabagua wala kuwanyanyapaa.