Baadhi ya michezo ambayo inaongoza hadi sasa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mikono (handball), mpira wa pete pamoja na riadha.
Katika michezo iliyofanyika jana tarehe 11 Agosti 25, kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu timu ya Ngome ilifanikiwa kuifunga timu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) goli 1-0 mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung.

Mchezo mwingine ulikuwa ni mpira wa kikapu uliozikutanisha timu za Ngome na JKT ambapo Ngome iliibuka kidedea kwa kuichapa JKT alama 81 dhidi ya 57.
Kwa upande wa mchezo wa wavu uliozikutanisha timu za Ngome na Polisi katika uwanja wa Amani, Ngome ilishinda jumla ya seti 3-0 na kuzidi kujiweka nafasi ya kufanya vizuri.
Kwa upande wa mchezo wa riadha, timu ya Ngome imeendelea kuongoza Mita 100 fainali ya wanawake na kufuzu medali ya dhahabu huku timu ya riadha Ngome Wanawake Mita 5000 ikishika nafasi ya kwanza, na pia timu ya riadha Ngome wanaume na Wanawake Mita 10,000 .
Matokeo haya yanaipa timu ya Ngome kuwa na uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa wa mshindi wa jumla.
Related