NJE ya Uwanja wa Benjamin Mkapa mambo yameanza kunoga kwa mashabiki wa Yanga kuonekana kwa wingi wakiwa wanashuka kutoka kwenye mabasi na usafiri mwingine ili kuingia kushuhudia tamasha la kilele cha wiki ya Mwananchi.
Tamasha hilo ambalo ni la saba kwa Yanga tangu lianzishwe mwaka 2019 chini ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Dr Mshindo Msolla na aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Mwinyi Zahera, linazidi kuvutia mashabiki ndani na nje ya nchi.
Katika tamasha hilo mbali na burudani za wasanii lakini kubwa ni utambulisho wa wachezaji wa msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuanza Septemba 17.
Yanga pia itacheza dhidi ya Bandari FC ikiwa ni mchezo wa kirafiki baada ya utambulisho wa mastaa wao, utakaoanza saa 11:00 jioni.