Na: Calvin Gwabara – Dodoma.
Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa
Sheria (OCPD) imekabidhi Juzuu za toleo la Urekebu wa Sheria la mwaka 2023 kwa
Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na kupongeza mchango mkubwa uliotolewa na Ofisi
hiyo kupitia watumishi wake kwenye utekelezaji wa zoezi la Urekebu.
“Wakati tunaanza zoezi hili Ofisi
yetu ilikuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa watumishi hasa Mawakili wa kufanya
kazi hii lakini tulikuwa tukibisha hodi kwenye Ofisi yako kuomba Mawakili kuja
kushirikiana nasi katika kutekeleza zoezi hili, na hakika walitusaidia sana
hadi tumekamilisha” alieleza Bi Katuga.
Aliongeza“ Ofisi ya Mwandishi
Mkuu wa Sheria kwa kutambua mchango wenu imeona ni muhimu na Ofisi yako pia
ipate nakala hizi ingawa tunatambua kuwa tumeleta chache kutokana na gharama
lakini ziwasaidie kwa kuanzia na kuwa kama kumbukumbu kwenu, lakini mnaweza
kupata nakala laini zote kupitia mfumo wa OAG MIS library” Alieleza Bi. Katuga.
Kaimu Mkurugenzi huyo wa
Divisheni ya Urekebu,Tafiti na Mafunzo ameongeza kuwa pamoja na nakala hizo
tano pia wameipatia Ofisi hiyo tuzo maalumu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kwa lengo la kutambua mchango wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka katika
zoezi hilo la Urekebu wa Sheria.
Akizungumza kwa niaba ya
watumishi wa Ofisi yake Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu
amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) na kushukuru kwa kuwapatia nakala hizo za kuanzia kwaajili
ya Ofisi yake maana wangeenda kununua dukani ingekuwa gharama kubwa.
“Ofisi yetu tunatumia Sheria
hizi kila siku maana tunatoa huduma za mashitaka kwenye mahakama zote nchini
hasa hasa mahakama za Wilaya na za Hakimu Mkazi ndiko tunaenda huko kila
siku,lakini pia mahakama kuu na mahakama ya Rufaa, kwahiyo hizi Sheria ni
nyenzo muhimu sana kwetu” Alieleza Bwana Mwakitalu.
Aliongeza” Nakala hizi
tulizozipata tutazisambaza kwa Mawakili wetu kwanza, alafu sisi tutaendela
kusubiria kupata zingine kwa utaratibu maalumu lakini pia kwa kutumia zle
ambazo zinazopatikana kwenye mfumo kwa nakala tepe”.
Toleo la Urekebu wa Sheria la
Mwaka 2023 lilizinduliwa na kwa mujibu wa Sheria na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwezi wan ne mwaka huu na
kutangaza kuanza kutumika tarehe 1/07/2025 na hivyo kufuta Toleo la sheria la
mwaka mwaka 2002.
![]() |
Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu akitoaa neno la shukrani kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria. |
![]() |
Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu pamoja na maafisa wengine wa ofisi yake wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo ofisini kwake. |
![]() |
Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu akifurahia moja ya juzuu alizokabidhiwa. |
![]() |
Picha ya pamoja ya Maafisa wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria mara baada ya hafla hiyo. |
Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Urekebu,Tafiti na Mafunzo Bi. Rehema Katuga akionesha moja ya juzuu hizo za toleo la Urekebu wa sheria za Mwaka 2023.