Simba nao wamo Mwananchi Day

LICHA ya mashabiki wa Yanga kuendelea kumiminika kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kushuhudia Kilele cha Wiki ya Mwananchi, lakini wale wa Simba nao wamo kujionea sherehe hizo za watani zao.

Simba ambao tamasha lao lilifanyika juzi, Jumatano, lakini baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wameonekana wakiingia uwanjani huku wakitaja msemo wao maarufu wa Ubaya Ubwele.

Hadi sasa watu wameingia kwa wingi uwanjani licha ya jua kali na ujio wa mashabiki hao wachache wa Simba haukuharibu amani na wameonekana sambamba na wenzao wa Yanga ambao ndio wenyeji wa tamasha hilo.

Leo katika uwanja huo, kunafanyika tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi na kutakuwepo na wasanii mbalimbali kusindikiza shamrashamra hizo wakiongozwa na Zuchu.