DK.BASHIRU ATOA RAI KWA WAZEE ,WATU MASHUHURI KUSAKA KURA ZA DK.SAMIA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Tabora

KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za mgombea urais wa Chama hicho Dk.Bashiru Ali ametoa wito kwa mabaraza ya wazee na watu mashuhuri kuendelea kumuombea kura Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu.

Dk.Bashiru ametoa mwito huo alipokuwa akizungumza mbele ya Dk.Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Nanenane Ipuli mkoani Tabora ambapo maelfu ya wananchi wa mkoa huo wamejitokeza kwa wingi.

“Moja ya maelezo ya Katibu Mkuu Dk.Asha Rose Migiro kwanza ni kuwaomba wana Tabora kutunza historia muhimu kwa Chama chetu na nchi yetu kwa kuendelea kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi.

“Maelekezo ya pili ni kwamba kupitia mabaraza ya wazee na watu mashuhuri tuwaombe waendelee kuwashawishi Watanzania waendelee kuwa na imani na chama cha Mapinduzi na waendelee kuwa na imanna mgombea wa ccm kwa ngazi ya urais.

“Sina mashaka mabaraza hayo ya wazee yatafanya kazi hiyo na kwa niaba ya wazee ningependa kuwataja wazee wawili wa hapa Tabora mmoja amenipigia simu anaitwa Stiven Mashishanga amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora ana miaka 91 anasema anakuombea kura hapo alipo”

“Mzee wapili anaitwa Nasoro Hamdani wana Tabora mnamjua ana umri si chini ya miaka 85 na amewahi amekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kutoka Tabora,amesema Dk.Bashiru

Hata hivyo amesema mwenyekiti wa CCM na mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan ameshatoa maelekezo kwake(Dk.Bashiru) aende kumsalimia na akamuombe kura kwa niaba yake.

“Nakuhakikishia baada ya wewe kuondoka nitabaki apa Tabora na nitaonana naye kutambua mchango wake kumpa pole ya maradhi lakini kumuomba kura”

“Kwahiyo tunapozungumza vijana mnajambo lenu,kina mama mnajambo lenu ,wazazi mna jambo lenu basi hata wazee wana jambo lao.Nimefanya kazi za uongozi katika chama na nimefanya kazi za uongozi wa Serikali katika muda mfupi.

“Nimefanya kazi za uongozi bungeni uzee dawa, kwahiyo wale wanaoupa hasira na wanakuwa na wasiwasi, wana mawazo tofauti,mikakati tofauti ,wana mikakati ya kiukombozi wasiende peke yao waende wapate busara za wazee.

“Na nyie wagombea wa Chama Cha Mapinduzi fuateni nyayo za mgombea wetu wa urais Dk.Samia kuwasikiliza wazee,”amesema Dk.Bashiru ambaye pia ametumia nafasi kuwashauri kufuata ushauri wa wazee.”

Amesisitiza kuwa : “Ninachotaka kuhimiza vijana mnapopata dhamana na wenye umri wakati tusiende peke yetu ,busara za wazee ni muhimu sana.”

Awali akiuzungumzia mkoa wa Tabora Dk.Bashiru amesema mwaka 1958 katika huo Chama cha TANU kilifanya Mkutano mkuu na kikafanya uamuzi unaojulikana uamuzi wa busara .

“Uamuzi ule ulikuwa unatishia umoja wa Chama Cha TANU na uamuzi ule ulikuwa unahusu haki ya Watanzania wote wakati huo watanganyika kupiga kura bila kujali hali zao,rangi zao na utambulisho wao .Kwahiyo wana Tabora lindeni historia hiyo na hazina ya busara.”