Anaandika Mshititi Dkt.Ahmad Sovu
MGOMBEA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)kwa nafasi ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ambaye anaendelea na kampeni za kusaka kura na leo Septemba 13 anatarajia kuanza ziara ya mikutano ya kampeni za kuomba kura kuelekea Uchqguzi Mkuu Oktoba 25,2025.
Udadisi wa Mshtiti katika mitaa na viunga vya mji anuwai wa Kigoma imeonesha namna wananchi walivyo na ari, shauku, hamu, ghamu ya kumpokea mgombea huyo shupavu na imara katika siasa za Tanzania.
NEEMA ZAKE KUU 10 KWA WANA KIGOMA
Wananchi hao wameeleza kinaga ubaga kuwa, katika kura ambazo watazi rundika (piga kwa wingi) ni za Rais Dkt.Samia.
Wamesema Mama Samia tangu amekuwa Rais amewafanyia mambo makubwa mengi na bado wana matarajio nae makubwa katika kuyakamilisha.
Kwa mapenzi na mahaba makubwa kwa Rais Samia yanayotokana na jitihada zake kubwa za kuuletea maendeleo mkoa wa Kigoma. Tutamlipa kwa mapokezi ya heshima, kibabe na kishindo_ Alisema mmoja wa wakazi wa mkoa huo.
Mambo hayo 10 ni yafuatayo;
Neema ya 1, Kuufanya mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara katika ukanda huu wa Magharibi na maziwa makuu
Tangu ameeingia madarakani Rais Samia Suluhu Hassan alionesha wazi dhamira yake ya kuufanya mkoa wa Kigoma sio tu kuwa Kituo cha biashara, bali kuwa kitovu cha Biashara kwa ukanda huu wa Magharibi kwa kuwa Kigoma inabebwa na Jiografia yake yenyewe.
Katika kufikia azma hiyo, ndio mana serikali yake tayari imefanya juhudi za kuunganisha mkoa wa Kigoma kwenye gridi Taifa, ujenzi meli mpya, barabara, meli na Kuboresha kiwanja cha ndege cha Kigoma.
Neema ya pili ni ujenzi wa Vyuo Vikuu ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amemwaga fedha mkoa wa Kigoma katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Tiba Muhimbili katika mkoa wa Kigoma (MUHAS), Chuo cha Uhasibu (TIA) na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Kujengwa kwa vyuo vikuu hivi sio tu kuwa vitaleta chachu ya elimu pia vitachagiza mzunguko wa uchumi na upatikanaji wa fedha.
Neema ya tatu kwa wana Kigoma ni maboresho ya hospitali ya rufaa ya Maweni na ujenzi wa Hospitali ya kanda.
Katika kuendeleza na kukuza afya za wananchi wa Kigoma Mheshimiwa Rais Samia aliongeza bajeti ya maboresho zaidi ya Maweni na anatarajiwa kujenga hospitali ya rufaa ya Kanda.
Neema ya 4 ni ujenzi wa Shule ya kisasa ya Wasichana Kigoma Girls.Katika kuwahakikishia elimu bora vijana. Dkt.Samia amejenga shule hiyo katika wilaya ya Uvinza. Shule hasa yenye hadhi kwa hakika ππ
Neema ya 5 ni Ujenzi wa Barabara na soko zuri la Kisasa la Mwanga ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amewezesha ujenzi wa barabara za njia nne ,bandari eneo la Kibirizi na Ujiji. Huyu ndio Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Neema ya 6 kwa wananchi wa Mkoa wa Kogoma ni Ujenzi wa kituo cha pamoja Mnanira Kigoma.
Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi kujenga One stop center katika eneo la Mnanira ili kurahisisha masuala mbalimbali katika ya Tanzania na nchi jirani. Tunapoandika hapa tayari mkandarasi yupo site na kazi imeanza.
Wakati Neema ya saba ni Bonde la Luiche ambapo Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza kilimo hususan kilimo cha umwagiliaji. Serikali yake imetoa zaidi ya Bilioni 60 kuhakikisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Luiche unafanikiwa.
Neema ya nane ni Kuunganisha mkoa wa Kigoma na Gridi ya Taifa.
Dkt. Samia Suluhu katika kufanikisha azma ya Kigoma ya kuwa KITOVU cha uchumi katika ukanda wa Magharibi. Tayari ameuunganisha mkoa wote wa Kigoma na Gridi ya Taifa.
Neema ya tisa ni Vitambulisho vya Taifa NIDA kwani Rais Samia Suluhu Hassan tayari amekamilisha ahadi ya Vitambulisho vya Taifa. Ambapo wananchi wengi wamepata Vitambulisho hivyo.
Neema ya 10 ni Ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kigoma na ujenzi wa soko la Katonga kupitia mradi wa TACTIC
Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa msingi mzuri wa Diplomasia ya Kiuchumi ya kimataifa na kuendeleza kulinda amani na utulivu. Mkoa wa Kigoma umenufaika na mradi wa TACTIC ambapo;
(i) Shilingi Bilioni 9.2-zitajenga na kukarabati soko la Mwanga na Katonga
(ii) Shilingi Bilioni 3.2 zinaendelea kufanya upanuzi wa barabara ya Wafipa Kagera na ujenzi wa daraja Mto Luiche
(iii) Shilingi Bilioni 8.6 Ujenzi unaoendelea wa Barabara ya Bangwe Ujiji Kilomita 7.5
(iv) Shilingi Bilioni 7.5 ujenzi wa barabara ya Old Kasulu yenye urefu wa Kilomita 6.5 kwa kiwango cha lami.
(v) Shilingi Bilioni 5.6 kujenga mifereji itakayopitisha maji katika mitaa ya Bangwe, Burega, Rutale, Mlole, Bushabani, mjimwema pamoja na Katonyanga
Hizi ndizo miongoni tu mwa baadhi ya neema 10 za Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mkoa wa Kigoma.
Ni kwa NEEMA hizi ndio maana wana Kigoma wamesema watampokea kibabe na kwa heshima Dkt.Samia na ifikapo Oktoba 29 wata β β β kwake na kwa wagombea wa CCM.
Kwani wana matarajio zaidi ya
-ukamilishaji wa ukarabati wa meli za mv.Liemba,mwongozo na ujenzi wa cherezo n.k
-Ujenzi wa Barabara ya Mpanda Kigoma
-Uhakika wa utulivu katika shughuli za uvuvi ziwa TANGANYIKA
-Kuchapuka kwa biashara ya Congo na nchi jirani.n.k
TURASHASHE, KARIBU KWAKO KIGOMA, NJOO KIFUA MBELE MAMA, WAHA NA WAMANYEMA WENZIO WAPO READY KUTIKI
Karibu tena Kigoma Pwani ya Bara.πΉπΏπΉπΏ
sovu82@gmail.com
0713400079.