PIGABET YAWAZAWADIA WASHINDI KUPITIA KAMPENI ZA KILA WIKI


 Dar es Salaam  Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Pigabet imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwazawadia wateja wake kupitia kampeni kabambe zinazofanyika kila wiki kwa wateja nchini kote.

Katika hafla ya hivi karibuni, Hemed Misonge, mhudumu kutoka Pigabet, aliungana na washindi wa promosheni hizo kwa kuwapatia zawadi nono zikiwemo:

Smartphone Samsung Galaxy A26 5G kupitia kampeni ya Jismartishe na Mixx by Yas

Hisense Smart TV 55” kupitia kampeni ya Shinda Ndinga

Washindi hao walipokea zawadi zao mbele ya viongozi wa Pigabet wakiwemo Suzan Joseph, Mhazini wa Kampuni na James Vedastus, Afisa Masoko, ambao walisisitiza kuwa promosheni hizi ni sehemu ya mkakati wa Pigabet wa kuwarudishia thamani wateja wake.

 “Tunafurahia kuona wateja wetu wakinufaika moja kwa moja kupitia promosheni hizi. Ni mwanzo tu, kwani kila wiki tunatoa nafasi mpya za ushindi kwa kila mteja,” alisema Hemed Misonge wakati wa makabidhiano.

Pigabet imekuwa ikiendesha kampeni zake kwa usawa kote nchini, na inatarajiwa kuendelea na msimu wa promosheni zinazosisimua zaidi katika siku zijazo.