Mgombea Ubunge wa Jimbo la Rufiji kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Mchengerwa, amewasili katika Viwanja vya Ujamaa leo Jumamosi, Septemba 13, 2025, kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Mchengerwa alipokelewa kwa shangwe na kusalimiana na wananchi pamoja na wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo muhimu.
Uzinduzi huo ni sehemu ya mikakati ya chama hicho kujinadi kwa wananchi na kuwaomba kura kwa ajili ya ushindi wa kishindo katika ngazi ya urais, ubunge na udiwani.
Related