Leo, 14.09.2025, Mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia CCM Mhe. Angellah Kairuki awapigia goti wananchi wa Kata ya Kwembe na Msigani kuwaomba kura za Mgombea Urais kupitia CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akieleza mambo makubwa yaliyofanywa na Dkt. Samia ndani ya Jimbo la Kibamba.
Mhe. Kairuki alielezea miradi ya kimkakati aliyoifanya Dkt. Samia kwenye Kata ya Kwembe ikiwemo ujenzi wa Shule ya kisasa ya Sayansi ya mabinti iliyopo Kata ya Kwembe, Miradi ya Maji inayoinufaisha Kwembe, mipango ya kutengeneza barabara, vituo vya afya e.t.c
Wananchi kwa furaha kubwa na kwa umoja wao wameahidi Oktoba WanaTiki kwa Mhe. Dkt. Samia, Kwa Mbuge Mhe. Kairuki na kwa Diwani wa CCM.
Wananchi wamempongeza Mhe. Kairuki kwa kuendelea kufanya siasa za kistaarabu huku wakionyesha matumaini makubwa mno kwake kwakuwa anauzoefu mkubwa ndani ya Bunge na Serikalini.