NYUMBANI KWA BABA LEVO WAMEAMUA KUMHESHIMISHA DK SAMIA…NYOMI LA KUFA MTU MAPAAAAAAAAAAA

Na Said Mwishehe,Mich

NYUMBANI kwa Baba Levo wameamua kwani leo kwani asubuhi hii uelekeo wa wananchi ni Uwanja wa Katosho uliopo Kigoma Mjini ambako ambapo mgombea urais kupitia

CCM atafanya mkutano wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29.

Tayari asubuhi uwanja wa Katoshi umefurika,misusuru ya wananchi ikiwa yote uelekeo wao ni ulipo mkutano wa Dk.Samia ambaye kwa hakika Kigoma kwa kauli zao wenyewe bila kushurutishwa wanasema Oktoba TUNATIKI kwa Samia.

Kigoma Mjini ndiko ambako katika Uchaguzi Mkuu ,CCM imesimamisha Clayton Chipando maarufu kwa jina la Baba Levo ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa akikishuru Chama hicho kwa kumheshimisha kwa kumpitisha kuwa mgombea ubunge Kigoma Mjini na ahadi yake ni kuhakikisha wana Kigoma wanampigia kura Dk.Samia ili ashinde kwa kishindo.

Hata hivyo katika Uwanja wa Katosho wakati mgombea urais CCM akisubiriwa burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali maarufu waendelea kutoa burudani.

Burudani pendwa zilizoporomoshwa kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao walifanya maelfu ya wananchi kukonga mioyo yao.

Wasanii hao ni Barnaba, barobaro na nyota wa muziki wa mduara, Nyota Waziri.