Vodacom Tanzania yazindua Dira ya 2030, yawekeza zaidi ya dola 100 milioni uboreshaji miundombinu ya teknolojia kwa uchumi jumuishi wa kidijitali

Kampuni ya Teknolojia na Mawasiliano, Vodacom Tanzania inapoadhimisha miaka 25 ya huduma hapa nchini imeweka msingi wa kizazi kijacho kwa kutangaza mpango wa kisasa wa teknolojia wenye thamani ya zaidi ya dola 100m ikiwa ni moja ya uwekezaji mkubwa zaidi wa miundombinu katika historia yake.

Mpango huu wa kihistoria unalenga kubadilisha hali ya mtandao nchini kwa kuboresha huduma na kuharakisha ujumuishaji wa kidijitali katika miji na maeneo ya vijijini yaliyo pembezoni, hivyo kuunga mkono ukuaji wa taifa kwa miaka 25 ijayo na zaidi.

Uboreshaji huu unajumuisha maboresho kwa maelfu ya minara ya kampuni hiyo ikiambatana miundombinu ya TEHAMA, ikiwemo jukwaa la M-Pesa. Maboresho haya yatawezesha kasi ya juu ya data, ubora wa simu za sauti, huduma adhimu za M-Pesa na pia kuimarisha usalama wa mtandao, yote haya yakijibu mahitaji ya watumiaji wa kampuni hiyo wanaoongezeka kila uchao.

“Safari yetu kuelekea Dira ya 2030 imeanza rasmi,” alisema Philip Besiimire, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, “kupitia uwekezaji huu, tunaweka msingi wa miaka mitano ijayo na zaidi, ili kuwawezesha wateja wetu kupata huduma bora zaidi, kulinda mazingira kupitia teknolojia rafiki kwa mazingira na kudumisha imani ya wateja wetu, washirika na wawekezaji. Hadi sasa, zaidi ya minara 1000 imeboreshwa katika kanda ya ziwa, nyanda za juu kusini na sehemu ya kanda ya hapa nchini.”

Mpango huu wa kisasa unaunga mkono Dira ya mwaka 2030 ya Vodacom Tanzania, ambayo inaweka watu, sayari na kuaminiwa kwa kampuni kuwa msingi wa kila uamuzi unaofanywa. Pia imejipambanua na ajenda ya kitaifa ya mabadiliko ya kidijitali ya nayoendelea hapa nchini, huku ikiangazia malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

Kwa kuzingatia lengo la kampuni la kupungiuza matumizi ya nishati zisizorejesheka (Net Zero 2035), uboreshaji wa mtandao wa Vodacom Tanzania utaanzisha miundombinu yenye ufanisi mzuri wa nishati ikipunguza matumizi ya umeme kwa hadi asilimia 30 huku ikiboresha utendaji na upatikanaji wa mtandao wake. Hatua hii inaendeleza dhamira ya kampuni hiyo katika masuala ya mazingira, jamii na utawala bora (ESG) huku ikihakikisha upatikanaji wa huduma bora za kidijitali kwa maeneo ya mijini na ya vijijini.

“Uboreshaji huu unahusisha teknolojia ya kisasa na utaongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa mtandao wa 4G, kuhakikisha kasi ya juu ya intaneti na muunganiko bora popote ambapo Vodacom inapatikana. Tunaelekea kwenye teknolojia rafiki kwa mazingira kwa kutumia teknolojia ya Huawei ya ‘zero-bit-zero watt’, ubunifu unaoongeza ufanisi wa matumizi ya nishati huku ukipunguza uzalishaji wa kaboni, na wakati huo huo kuboresha utendaji wa 4G na 5G,” alisema Mkurugenzi wa Mtandao (Network Director) wa kampuni hiyo Andrew Lupembe

Aliongeza kwamba zaidi ya hayo, wanaboresha matumizi ya nafasi kwenye minara kwa kuanzisha teknolojia ya redio ya masafa mengi inayowezesha masafa yote kutumia redio moja pamoja na kuunganisha masafa mbalimbali kwenye antena moja.

Kadri uchumi wa kidijitali wa Tanzania unavyoendelea kukua, Vodacom Tanzania inaongeza juhudi zake kama mwezeshaji, ikiharakisha ujumuishaji wa kidijitali na kifedha, kuchochea ubunifu, na kuwekeza katika miundombinu inayowaunganisha Watanzania wote na fursa mbalimbali zinazopatikana katika kipindi hicho.
Mtaalamu wa mafunzo na vijana kutoka Vodacom Tanzania Plc,Bw Samwel Komba akimkabidhi cheti Mwanafunzi Doris Nisetasi, mhitimu wa mafunzo ya programu ya ‘Code Like A Girl’ yenye lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) ambayo inafadhiliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab katika hafla iliyofanyika ijumaa jijini Dar es Salaam

Graduate of the Coding program, Lairati Yahya, presenting her group’s project during the climax of the Code Like a Girl training in Dar es Salaam. The program is run by dLab with sponsorship from Vodacom Tanzania PLC, aiming to educate and inspire girls to pursue studies in Science, Technology, Engineering, and Mathematics (STEM). So far, more than 3,370 girls have graduated from this training in the country.