……………
Kamanda wa Jeshi hilo
Muliro Muliro amesema hayo jijini Dar es salaam amesema Tukio hilo limetokea Septemba 11, 2025, wakati askari waliokuwa doria walipomtilia mashaka mtu huyo na kufuatilia mienendo yake hadi alipokamatwa.
Mtuhumiwa huyo, aliyefahamika kwa jina la Peter Mahende, mkazi wa Ilemela mkoani Mwanza, alikutwa akiwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi baadhi ya wafanyabiashara wa eneo hilo kinyume na taratibu za kisheria. Taarifa za awali zinaeleza kuwa Mahende hakuwa na nyaraka zozote halali zinazoonesha kuwa ni askari halisi wa Jeshi la Polisi.
Kwa sasa, mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi, na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwanasa watuhumiwa sita wanaodaiwa kuhusika na kupokea pamoja na kubadilisha mifumo ya simu za mkononi zinazodaiwa kuwa za wizi.
Jumla ya simu 55 na kompyuta mpakato saba (07) zimeripotiwa kupatikana mikononi mwa watuhumiwa hao, ambao inadaiwa walikuwa wakizibadilisha ili kuficha asili yake halisi.
Watuhumiwa waliokamatwa ni Peter Chambo, mkazi wa Tabata; Ally Shemela, mkazi wa Tabata; Mudrick Alkharous, mkazi wa Temeke; Nestory Lucas, mkazi wa Kimara Matosa; Said Hassan, mkazi wa Mbezi; na Saidi Kisaka, mkazi wa Tabata. Inadaiwa kuwa mtandao huu wa kihalifu ulikuwa ukihusika katika usambazaji wa vifaa vya kielektroniki vilivyoibiwa kwa njia za udanganyifu.