DKT. MWINYI: UWANJA MPYA WA NDEGE PEMBA UNAKUJA

MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inatarajia kumkabidhi Mkandarasi Mkataba wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba ifikapo Septemba 25 mwaka huu.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 15 Septemba 2025 katika Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Kisiwani Pemba, uliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.


Kukamilika kwa uwanja huo wa kisasa kutaiweka Pemba juu kiutalii na kiuchumi kwani ndege kubwa zitatuwa moja kwa moja Pemba.
📌Maendeleo aliyoyagusia leo Pemba:

✅ Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kisasa Pemba
✅ Hati miliki kwa mashamba ya karafuu
✅ Barabara ya Chake Chake – Mkoani kukamilika
✅ Nyumba 10,000 za gharama nafuu Unguja na Pemba
✅ Kuimarisha uwekezaji na viwanda ili kuongeza ajira kwa vijana
Dkt. Mwinyi amewaomba wananchi wa Pemba kumpa tena ridhaa ya kuongoza Zanzibar na pia kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wabunge, wawakilishi na madiwani wa CCM.
💚 CCM itaendelea kuhubiri amani, mshikamano na kuendesha kampeni za kiistarabu.