MOI YAZINDUA MFUMO MPYA WA KUWEKA MIADI KWA MADAKTARI (MOI ONLINE APPOINTMENT SYSTEM)

 :::::::::::

Na Matha Kimaro- MOI 

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), imezindua rasmi mfumo mpya wa kuweka miadi na madaktari wa taasisi hiyo ujulikanao kama “MOI Online appointment system “ ambao humsaidia mgonjwa kuweka miadi ya kuonana na daktari anayemtaka, muda na klinki kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika MOI.

Uzinduzi huo umefanyika leo 

“Mgonjwa baada ya kufanya miadi atapokea ujumbe mfupi wa simu ukimtaarifu kukubalika kwa miadi yake, na hata pale daktari husika atakapopata udhuru mteja atapata taarifa kwenye simu yake na kumwezesha kuchagua daktari mwingine au amsubirie kwa siku nyingine”

Amesema mfumo huo mpya unapatikana saa 24 kwa kutumia simu janja, komyuta mpakato au kishikwambi kupitia tovuti kuu ya taasisi www.moi.ac.tz au kiunganishi https://onlineappointment.moi.ac.tz/appointment/ ambapo mgonjwa atalazimika kujaza taarifa zake fupi na kisha kuwalisha.

“Tumejipanga kutoa huduma bora kwa kwa kuokoa muda wa mgonjwa kusubiri kumuona daktari, hii haina maana wagonjwa ambao hawajaweka miadi kwa mfumo huu hawatahudumiwa kwa wakati…wagonjwa wote watapata huduma kama kawaida isipokuwa mfumo huu mpya unampa uhakika wa mgonjwa kupata huduma kwa wakati na uhakika zaidi” amefafanua Dkt. Mpoki