Msafara wa Dkt. Nchimbi Wasimamishwa na Wakazi wa Mombo-Tanga – Global Publishers



Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, umesimamishwa na wananchi wa Mombo leo Jumatatu, Septemba
15, 2025.

Dkt. Nchimbi alikuwa akielekea Wilaya Korogwe Mjini kwa ajili ya kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni, lakini alilazimika kusimama baada ya wananchi wa Mombo kujitokeza kwa wingi barabarani kumpokea.

Akizungumza na wananchi hao, Dkt. Nchimbi aliwanadi wagombea wa CCM na aliendelea kuhamasisha wananchi kuhusu llani ya Uchaguzi уа ССМ 2025-2030, akieleza kuwa imekusudia kuboresha maisha ya Watanzania na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Dkt. Nchimbi alitumia fursa hiyo pia kuwaomba wananchi kumpigia kura kwa kishindo Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wabunge na madiwani wa chama hicho ifikapo Oktoba 29, 2025.