BAADA ya kiungo wa zamani wa Simba, Fabrice Ngoma kusaini mwaka Al-Nasr ya Libya, amesema maisha ya mwanasoka ni popote na kinachotakiwa ni kutunza kiwango na nidhamu ya kazi.
Ngoma aliitumikia Simba misimu miwili wa kwanza wa 2023/24 alimaliza na mabao matatu na 2024/25 alimaliza na mabao manne, kisha ikaachana naye na katika nafasi yake walisajiliwa Alassane Kante, Charles Semfuko pia Naby Camara aliye na uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja.
“Mchezaji anatakiwa kulinda kiwango chake na kuzingatia nidhamu ya kazi, kwani leo anaweza akacheza timu fulani na kesho akaenda nyingine, wanachokiangalia viongozi ama makocha ni huduma yake iwe na mchango mkubwa,” alisema Ngoma na kuongeza;
“Naanza maisha mengine mapya na klabu ya Al-Nasr, hadi inanisajili iliona huduma yangu muhimu kwao, lazima nijipange kuhakikisha nakifanya kile wanachokitarajia kutoka kwangu.”
Alisema mchezaji yeyote anayetaka kufika mbali, katika kazi yake ya mpira wa miguu lazima akili yake izingatie timu inachohitaji kutoka kwake na akifanye kwa bidii:
“Mnapokuwa katika timu lengo ni moja tu ni kutimiza malengo inayokuwa imejiwekea.”