DKT.NCHIMBI AOMBA WANANCHI HANDENI KUICHAGUA CCM KWA KURA NYINGI ILI ISHINDE KWA KISHINDO UCHAGUZI MKUU.

MGOMBEA Urais mwenza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaomba wananchi wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kukipigia kura Chama hicho ili kishinde kwa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

Ametoa ombi hilo alipokuwa akihutubia maelfu ya Wananchi waliofika kumsikiliza,katika uwanja wa Kigoda leo Septemba 15, 2025 wilayani Handeni ambapo ameendelea na mikutano ya kampeni kuomba kura za mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan,wabunge na madiwani.

Dkt.Nchimbi ameanza siku yake ya kwanza mkoani Tanga kufanya mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025,na mpaka sasa tayari ameshafanya mikutano yake ya kampeni ndani ya mikoa 11 mpaka sasa.