MTEULE wa Viti Maalumu vya Ubunge katika Mkoa wa Kigoma, Beng’i Issa amewakata wanawake wa Mkoa huo, kuwa na matumaini makubwa kupata uwezeshaji wa kiuchumi kwa fedha zilizotengwa na serikali sh. bilioni 200.
Akizungumza mkoani humo, amesema serikali ya Rais Dk.Samia imekuwa mistari wa mbele katika kujali makundi yote ya wananchi hususan kuwawesesha kiuchumi.
Alisema kwa mantiki hiyo, ndiyo maana wanaendelea kutafuta kura za kishindo za Dk.Samia Mkoani kigoma kuhakikisha anaendelea kuongoza serikali.
“Nimeshiriki kutafuta kura za Mheshimiwa Rais kwenye majimbo ya Muhambwe Kibondo, Mahembe Kigoma vijijini _ Kaskazini, Kasulu Heru juu na Kigoma Mjini, wananchi wamekubali sera zetu wameahidi kumchagua kwa kishindo,”alisema.
