DOTTO NDUMBIKWA AAHIDI KUCHANGIA MADAWATI 50, MAGODORO 20 NA MBAO SHULE YA MSINGI MAZINYUNGU.

Farida Mangube, Kilosa
MDAU wa Maendeleo Wilayani Kilosa Ndugu Dotto Ndumbikwa ameahidi kuchangia Madawati Hamsini (50), Magodoro Ishirini (20), Pamoja na Mbao katika Ujenzi wa Shule ya Msingi Mazinyungu Wilayani Kilosa.
Ndugu Dotto ametoa ahadi hiyo wakati akijibu Risala ya Wanafunzi iliyoelezea baadhi ya Changamoto Shuleni hapo katika Mahafali ya kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka wa 2025.
Kwa upande mwengine Ndugu Dotto amelazimika kufanya harambee kwa wazazi wa Wanafunzi hao ili nao wawe sehemu ya kuchangia katika shughuli za Maendeleo.
Lakini pia Ndugu Dotto amewataka Wazazi na Walezi kusimamia Maadili ya Wanafunzi waliomaliza Darasa la saba ambao muda mwingi kwa kipindi kijacho watakua majumbani, hivyo Wazazi na walezi wanajukumu la kuhakikisha Wanafunzi hao wanabaki katika mstari hadi watakapoingia kidato cha kwanza.