Kikosi cha Mnyama wa Afrika Mashariki, Simba SC, kimewasili nchini Botswana kwaajili ya mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya wenyeji Gaborone United.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Septemba 20 kwenye Uwanja wa Obed Itani Chilume, ambapo mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya aina yake.
Simba SC inashuka dimbani ikiwa na dhamira ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri ugenini, ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua zinazofuata za michuano hii mikubwa barani Afrika.
Related