Mariam Ibrahim aungana na wanawake wa Pwani kufanya usafi Jimbo la Kibaha Vijijini

Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mariam Ibrahim, leo Septemba 18 ameungana na Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Pwani katika zoezi la kufagia viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani, Jimbo la Kibaha Vijijini, mkoani Pwani.

Mariam alishiriki shughuli hiyo kama sehemu ya maandalizi ya uzinduzi wa kampeni unaotarajiwa kufanyika kesho katika uwanja huo.