▫️Nusu fainali ya kwanza kufanyika usiku wa leo kwa mapambano 14
▫️Magereza warudi kwa kishindo msimu huu
18-09-2025, Tanga.
MASHINDANO ya ngumi Klabu Bingwa ya Taifa yamefikia hatu ya nusu fainali ambapo usiku wa leo jumla ya mapambano 14 yatapiganwa katika uwanja wa Urithi, Jijini Tanga.
Mapambano hayo yatawakutanisha jumla ya mabondia 27 ambapo mahasimu wanaochuana kwa ukaribu timu za MMJKT na Ngome zitawakilishwa na mabondia 6 kutoka kila timu huku Maaskari Magereza wakiwa wamecharuka msimu huu wakiwanyemelea kwa ukaribu kwa kuwa na wachezaji 5 watakaopambana usiku wa leo.
JKT Mgulani (Dsm) na Jeba Boxing (Tanga) wanafuatia kwa kuwa na mabondia 2 kwa kila timu huku Band Coy (Dsm), Ngamiani (Tanga) na Chang’ombe Boxing wakiwa na bondia 1 kutoka kila timu.
Mashindano haya yanatarajiwa kufikia hatua ya fainali na kumpata bingwa wa Taifa wa 2025 siku ya Jumamosi tarehe 21-09-2025.
📸 Matukio tofauti ya jana usiku katika mapambano ya robo fainali