WANANCHI WAENDELEA KUELIMISHWA UFUGAJI WA NYUKI

 Wananchi wanaendelea kuelimishwa  kuhusu ufugaji wa nyuki kuwa ni fursa kubwa ya kipato na maisha bora kwani nyuki wanatupa asali yenye thamani kubwa sokoni, lakini pia wanasaidia kuchavusha mazao yetu na kulinda uhai wa mazingira.

Ni muhimu wadau na wananchi mbalimbali kubadilika na kuacha kutumia moto wakati wa kuvuna asali kwani moto unaharibu mizinga, unaua nyuki na kuunguza misitu yetu, hivyo ukitumia mbinu hizo za kizamani zinapoteza siyo tu nyuki bali pia rasilimali muhimu za misitu na uoto wa asili.

Wananchi wanakumbushwa kuchagua mbinu za kisasa za kuvuna asali ambazo ni mbinu rahisi, salama na zinazohifadhi nyuki pamoja na mazingira yake. 

Aidha inasisitizwa  kuwa kutumia njia hizi zitalinda misitu na kuepelekea kupata asali bora zaidi na kuendelea kutunza misitu kwani utabaki urithi mzuri wa kijani kwa manufaa ya kizazi cha sasa na  vizazi vijavyo.