JUBILEE INSURANCE YAWAPATIA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MERU-ARUSHA BIMA YA AFYA BURE

 Na Mwandishi Wetu,Arusha.

Jubilee Insurance kupitia kampuni zake za Bima ya Afya na Maisha imezindua mpango wakusaidia jamii kwa kuwapatia wanafunzi 10 wa Shule ya Msingi Meru, Arusha, bima ya afya. 

Hatua hii inalenga kusaidia familia na watotokupata huduma bora za afya na kuendeleakuimarisha ustawi wa jamii.

Kwa kutoa bima hizo  Jubilee Insurance inalenga kuhakikisha watoto wanapata hudumabora za afya bila mzigo wa kifedha kwa wazaziwao, na pia kuchangia katika kuendeleza elimukwa kuwa na watoto wenye afya bora.



Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwwakilishi wa Jubilee Insurance alisema: “Tunayo furaha kuendelea kushirikiana na jamii katika kuhakikisha afya bora kwa vizazi vijavyo. 

“Watoto ni taifa la kesho na jukumu letu nikuwawezesha kusoma bila vikwazovinavyotokana na changamoto za kiafya.”



Amefafanua zaidi pia hatua hıyo ni sehemu ya mkakati wao  Jubilee Insurance wa kuimarisha ushirikiano na jamiikupitia mpango wa kurudisha kwa jamii, kwakuhakikisha afya na ustawi vinapewakipaumbele.