::::::::::
JUKWAA la kidijitali la PIKU Afrika, linaloendesha minada ya kipekee kupitia mtandao, limetangaza na kukabidhi zawadi kwa washindi wawili wa awamu ya nne ya promosheni yake ya minada ya kidijitali.
Katika hafla hiyo, washindi wawili bora waliibuka na zawadi mbalimbali kama ifuatavyo: Mshindi wa kwanza, Hamimu Madenge, Meneja wa Super Market ya Viva iliyopo Makumbusho jijini Dar es Salaam, alijishindia bidhaa zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili.
Mshindi wa pili, Adam Ahmad, mkazi wa Goba na muuzaji wa vifaa vya ujenzi, alijishindia simu janja aina ya Samsung, laini ya Airtel yenye kifurushi cha mwaka mzima pamoja na spika.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zake, Madenge alisema aliifahamu PIKU kupitia mteja wake mmoja wa dukani na alipomwelekeza jinsi ya kucheza alivutiwa na mnada huo Kisha kuamua kushiriki kwa dhati akiamini lazima ashinde.
“Nilipoanza kucheza nilijiambia moyoni hapa si jaribio, bali lazima nishinde. Niliweka fedha, nikapata tiketi za kutosha na kufanikiwa kushinda baadhi ya bidhaa zilizokuwepo katika mnada. Nimepokea zawadi zangu, hakika ni nzuri na zina ubora wa hali ya juu,” alisema Madenge.
Naye Ahmad alisema aliifahamu PIKU kupitia rafiki yake ambaye alijiunga na jukwaa hilo na marinate kufanikiwa kushinda hivyo aliamua na yeye kucheza ili ajipatie zawadi.
“Nilipojaribu nami nikabahatika kushinda simu ambayo nilikuwa nahitaji. PIKU si wadanganyifu, ni wa kweli kabisa, ukishinda unapewa bidhaa zako. Nawashauri watu washiriki na nao watajishindia,” alisema.
Kwa upande wa tiketi za kushiriki, PIKU Afrika imeweka viwango rahisi kama ifuatavyo, Tiketi 10 kwa Sh. 1,000, Tiketi 50 kwa Sh. 5,000, Tiketi 100 kwa Sh. 10,000 na Tiketi 1,000 kwa Sh. 100,000.
Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa PIKU Afrika, Barnabas Mbunda, alisisitiza kuwa kadri idadi ya tiketi inavyoongezeka, ndivyo nafasi ya kushinda inavyokuwa kubwa zaidi.
“Ili kuweza kuingia katika mnada huu unatakiwa kupakua App ya Piku katika play store au Apple Store, Kisha kufuata maelekezo, niwashauri watu waendelee kujiunga na kucheza kwani bidhaa za kushindaniwa bado zipo nyingi,” amesema
Mbunda ameongeza kuwa minada mikubwa inaendelea kushindaniwa ikiwemo gari aina ya Toyota Raum, Pikipiki mpya aina ya TVS pamoja na dhahabu.
Kwa mara nyingine, PIKU Afrika imeonesha kuwa kinara katika mapinduzi ya minada ya mtandaoni nchini, ikiwapa Watanzania fursa ya kupata bidhaa bora kwa bei nafuu kupitia mfumo wa kidijitali, wa uwazi na wa kipekee.