ONESHO LA JAPAN ‘I LOVE SUSHI’ LAZINDULIWA RASMI MAKUMBUSHO YA TAIFA

…………………

Onesho liitwalo ‘I Love Sushi’ lililoandaliwa na Ubalozi wa Japan nchini kwenye Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam limezinduliwa na Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Maliasili na Utalii, leo tarehe 19 Septemba 2025.

Onesho hilo limelenga kuonesha ustadi wa safari ya kihistoria ya miaka 1000 ya Sushi ambayo inatambulika na UNESCO kama Urithi wa Utamaduni usiyoshikika kutoka Japan.

Akiongea kwenye uzinduzi huo Balozi wa Japan, Mhe. Ueda Shoichi amesema Sushi ni chakula cha kiutamaduni ndani ya nchi ya Japani.

Akimwakilisha Mhe. Waziri, Dkt Noel Lwoga, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania alisema kwamba uzinduzi wa onesho hilo unatoa fursa kwa wananchi kujifunza urithi wa utamaduni wa mataifa mengine, unafundisha umuhimu wa uhifadhi wa urithi wa utamaduni, utapelekea ongezeko la watalii makumbusho, hasa kutoka Japan, na utaimarisha mashirikiano baina ya nchi ya Japan na Tanzania.

Onesho hilo litaendelea kuwepo mpaka tar 10 Oktoba 2025 katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.