VIBE LA WANA MBINGA KWA DK.SAMIA SI MCHEZO

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

HAKIKA wana Mbinga wana Vibe sio mchezo!Ndivyo unavyoweza kueleza kutokana na wingi wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni za mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Dk.Samia leo anapokelewa mkoani Ruvuma kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake na leo atatanya mikutano miwili ukiwemo wa Wilaya ya Mbinga na baadae atakuwa na mkutano Mbamba Bay .

Kwa wananchi wa Mbinga Mjini tayari wamefurika katika eneo lq mkutano wakimsubiria kwa hamu kubwa Dk.Samia Suluhu ambaye ameendelea kunadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030 pamoja na kuomba kura kwa wananchi.

Hata hivyo wananchi hao muda wote walionekana wakiwa na Shangwe(Vibe) la kutosha ,wako wanaoburudika kwa muziki kutoka kwa wasanii wanaotoa burudani.

Wakati burudani ikiendelea mabango yenye picha ya mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan yameupamba mji wa Mbinga.