BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA UNGA, NEW YORK MAREKANI

 

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Africa kuhusu Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama, Balozi Liberata Mulamula ameshiriki kwa mara ya kwanza kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kama mjumbe Mwakilishi wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo maalum unaofanyika New York nchini Marekani, una lengo la kutathimini Mkutano wa Wanawake wa Beijing baada ya miaka 30, kukiwa na mafanikio makubwa.

Kikao hicho maalum cha Siku moja kilichoanza leo tarehe 22 Septemba kuhusu miaka 30 ya Mkutano wa Beijing kumewakutanisha na kuhutubiwa na viongozi mbalimbali kutoka katika Mataifa yote Wanachama wa Umoja wa Mataifa.