TADB YACHOCHEA MAENDELEO YA KILIMO NA UFUGAJI KIGOMA

Na Mwandishi wetu

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewezesha  ujenzi wa Kiwanda cha Kuku wa mayai cha Mayai Ltd kinachomilikiwa na Bw. Rupinder Sandhu kimejengwa katika kijiji cha  Kimbwela, kata ya simbo, Mkoani Kigoma.

Akizungumzia Kiwanda hicho, Afisa Maendeleo ya Biashara toka  TADB Bwana Patrick D. Kapungu amesema Kiwanda hicho ni kikubwa katika Mikoa ya Kanda ya Magharibi inayojumuisha Kigoma,Tabora na Katavi na kinatoa ajira za kudumu pamoja na za muda  (vibarua) kwa wakazi  wa Kigoma hususani wale wa maeneo jirani na mradi pamoja na watanzania wengine kwa ujumla. 

Mpaka sasa kiwanda kimepata manufaa mengi ikiwa ni  pamoja na kutoa ajira kwa wananchi zaidi ya 40, kuimarishwa kwa huduma za jamii kama kuwajengea visima vya maji,  umeme, barabara, kuchangia katika ujenzi wa shule na hospitali kwa vijiji vinavyozunguka kiwanda hicho.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw.Rupinder  Sandhu amesema  asilimia 80 ya kiwanda hicho ni uwezeshaji kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), hivyo anaishkru sana Serikali  kuiwezesha TADB maana bila hivyo hasingeweza kufikia hatua hiyo.

Kiwanda hicho kinazalisha trei 3,000 za mayai sawa na trei 90,000 za mayai kwa mwezi haya ni mageuzi makubwa ya uchumi kupitia TADB.