WADAU MBALIMBALI WAPEWA ELIMU KATIKA BANDA LA TASAC

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeshiriki maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan vilivyopo mkoani Geita kuanzia tarehe 18 hadi 28 Septemba, 2025.

Wadau mbalimbali wametembelea banda la TASAC na kupata elimu ya ugomboaji wa bidhaa ikiwemo makinikia, vilipuzi na madawa yanayotumika kwenye migodi ya uchumbaji wa madini, elimu ya usalama, ulinzi wa vyombo vya usafiri majini na utunzaji wa mazingira ambamo vyombo vinafanyakazi imetolewa

TASAC imekuwa ikitumia fursa ya maonesho hayo kutoa elimu ya umuhimu wa huduma za usafirishaji majini, usalama wa vyombo vya usafiri majini, pamoja na fursa za biashara zinazopatikana kupitia sekta ya usafiri kwa njia ya maji

Aidha, Wadau waliotembelea banda hilo wamepongeza jitihada za Shirika katika kuelimisha Umma na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia usafirishaji wa majini.