DKT.NCHIMBI ATINGA JIMBO LA WANGING’OMBE KUSAKA KURA ZA USHINDI MZITO WA CCM

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi anaendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea urais wa chama hicho, Dkt.Samia Suluhu Hassan, za Wabunge na Madiwani, ambapo leo Septemba 23, 2025 ameingia siku ya pili ya kufanya mikutano ya kampeni mkoani Njombe.

Picha mbalimbali za Dk Nchimbi alipowasili katika mkutano wake wa kampeni unaofanyika katika Uwanja wa Igwachanya, wilayani Wanging’ombe.