Sababu mabango ya upinzani ‘kufunikwa’

Kampeni za uchaguzi zinahusisha njia nyingi zinazowafanya wananchi wahamasike kumchagua mgombea au chama fulani ambacho kitawafikia na kuwashawishi kwamba ndiyo kinastahili kuongoza Serikali. Moja ya njia hizo ni mikutano ya hadhara ambayo vyama vya siasa vinakwenda moja kwa moja kwa wananchi na kuwaeleza kuhusu ilani za vyama vyao na kuahidi mambo ambayo wakipewa ridhaa watayafanya…

Read More

NIKAMBIE MAMA: Wala rushwa katika sura ya hisani

Mtu wa Pwani anaweza kuuliza swali linalofanana na jibu: “Hapo pajani pajani?” Kama anayeulizwa ni wa kutoka bara anaweza kujibu: “Sasa kumbe ulifikiria pajani ni gotini?” Lakini kumbe anakuwa hajaelewa kabisa mwenzake anaulizia nini. Swali ni: “Hapo kwenye paja panakuja nini? Ni kama mtu aliyeona dalili ya kitu kisicho cha kawaida (labda kipele hivi) kwenye…

Read More

FYATU MFYATUZI: Walichagua mbung’o wakidhani mbunge!

Mbung’o, chafuo, au ndorobo au tsetse fly kwa kimasai ni mdudu asababishaye ugonjwa hatari wa malale kwa wanadamu na nagana kwa wanyama. Kama inzi wengine, mbung’o si hatari tu bali mchafu na mwenye kueneza maradhi mbali na kuchafua vyakula. Je, wajua mja aweza kuwa mbung’o? Kuna kisa kilitokea kwenye kaya ya Fyatuko. Katika kisa hiki,…

Read More