Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limemteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa shirikisho hilo kuanzia Oktoba 1, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, uteuzi wa Mirambo ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF unakuja kuchukua nafasi ya Kidao Wilfred ambaye mkataba wake unamalizika Septemba 30, 2025.
Mirambo ataanza rasmi majukumu yake mapya mara baada ya kuhitimishwa kwa mkataba wa Kidao, ambapo anatarajiwa kusimamia shughuli za kila siku za sekretarieti ya TFF hadi hapo uamuzi mwingine utakapofanywa na Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo.
Related