Kufuatia Uwanja wa Manungu Complex uliopo Morogoro kutokukidhi vigezo vinavyotakiwa ili utumike kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar imeuchagua Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa mechi za nyumbani za Ligi Kuu Bara.
Mtibwa Sugar iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu huu, imeanza kwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mashujaa ikiwa ugenini.
Timu hiyo baada ya kupoteza mechi ya kwanza, sasa itaikaribisha Fountain Gate, Septemba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Taarifa ya Mtibwa Sugar imesema: “Mchezo wetu unaofuata wa Ligi Kuu tunacheza dhidi ya Fountain Gate. Mchezo utachezwa Jumapili ya tarehe 28 saa 10:00 jioni uwanja wa Jamhuri Dodoma.
“Huu mchezo sisi ndio wenyeji na tumelazimika kupeleka Dodoma sababu ya marekebisho ya Uwanja wa Manungu ambao utakamilika hivi karibuni.”