MUHIMBILI YAKANUSHA KUWAFUTA KAZI WAFANYAKAZI 200


 ::::

Hospitali ya Taifa Muhimbili imekanusha taarifa inayosambaa mitandaoni kuwa imewafuta kazi wafanyakazi 200 kwa kuwa haina fedha za kuwalipa.

Taarifa iliyotolewa na hospitali hiyo imesema hadi kufikia Septemba 25, 2025, ina jumla ya wafanyakazi 4,326 ambapo wenye mikataba ya muda mfupi ni 251.

“Tangu Januari hadi Septemba 25, 2025, Hospitali imepokea wafanyakazi wa ajira mpya 380 wenye masharti ya kudumu na kadiri Hospitali inavyopokea wafanyakazi hao, ndivyo inavyopunguza wafanyakazi wenye ajira za mikataba (volunteers) kulingana na kada husika,” imesema.

Imeongeza kuwa “Katika kipindi hicho hicho, Hospitali ilitoa notisi ya kusitisha mikataba kwa wafanyakazi 27 waliokuwa na ajira za mikataba ya muda mfupi (volunteers).”