NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO AZINDUWA KONGAMANO LA 5 LA ELIMU BORA KIMATAIFA

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizinduwa Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akizungumza kwenye Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Viongozi mbalimbali na wageni wakiwa katika Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).



Viongozi mbalimbali na wageni wakiwa katika Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

Viongozi mbalimbali na wageni wakiwa katika Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).


Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Simon Nanyaro akizungumza kwenye Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).


Sehemu ya washiriki katika Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).


Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akizungumza kwenye Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameupongeza Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), kwa umoja na mshikamano wanaouonesha kwa wanachama wake na kushirikiana na Serikali katika kuleta maeneleo kwenye sekta ya elimu. Nguvu mnayoionesha katika umoja wenu katika kushirikiana na Serikali kuboresha elimu kama yalivyo maono yenu ni tafsiri tosha kuonesha mnavyoguswa na maendeleo ya elimu nchini.

Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa Kongamano la 5 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). Alisema jukumu la kuboresha elimu nchini si la Serikali tu, bali ni la wadau wote wa elimu kushirikiana na wizara husika katika kuboresha elimu.

“Leo hii tukiwa tunafungua Kongamano hili naomba kutumia fursa hii kuipongeza Wizara ya Elimu kwa kuwashirikisha vizuri wadau mbalimbali wa sekta ya elimu katika kuleta maendeleo, kitendo cha wizara ya elimu kuamua kuona kazi ya kuboresha elimu si kazi ya Serikali pekee bali kuhusisha wadau wengine ni jambo la kuigwa na taasisi nyingine za Serikali,” alisema.

“Niwapongeze pia TEN/MET kwa kuunganisha zaidi ya mashirika 245 kwa pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha jamii inapata elimu bora na si bora elimu kama inavyoonesha katika maono yenu. Napongeza mwendelezo wa kazi yenu hii ambapo inaonesha mmeanza tangu mwaka !999 hadi sasa mkiendelea kufanya kazi pamoja na kwa malengo mlojiwekea.” alisema kiongozi huyo.

Aidha alisema kufanyika kwa kongamano hilo kati ya sekta binafsi za wadau wa elimu pamoja na Serikali ni ishara ya kukubaliana kuwa elimu ni kipaumbele cha taifa, hivyo kuna kila sababu ya kuwekeza vya kutosha katika sekta hiyo muhimu nchini. 

Alisema ulimwengu tulionao kwa sasa ni ulimwengu wa kishindani unaobadilika kila wakati na ni ulimwengu wa sayansi, ulimwengu ambao kila mwenye maarifa atawashinda wasio kuwa na maarifa ni ulimwengu ambao hautaki kabisa kubahatisha bali usahihi wa kila jambo unalolifanya, ni ulimwengu ambao muda na wakati unathamani kubwa na ili iweze kuonekana elimu inaitaji kuwa kipaumbele uweze kufanikiwa.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala alisema Kongamano la 5 la Ubora wa elimu lililoshirikisha nchi zaidi ya 12 na taasisi anuai za elimu lengo kubwa la mkutano huo ni kujadili namna bora ya kuboresha ugemaji wa rasilimali za ndani kwenye sekta ya elimu.

Alisema unapozungumzia ugemaji wa rasilimali za ndani unaenda pamoja na rasilimali watu, fedha na vitu vingine vingi na kuangalia ni namna gani tunaweza kutumia kupunguza utegemezi kwa kutumia rasilimali hizo kuchangia maboresho ya elimu kwa kuwashirikisha wadau anuai wa sekta ya elimu. 

“…Yapo mabadiliko makubwa yamefanywa na Serikali katika kuboresha elimu yetu, lakini hayo mabadiliko yote yanaitaji rasilimali fedha, rasilimali watu na vinginevyo kuchangia maboresho…mfano sasa hivi Serikali inatoa elimu bila ada kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita kwa hiyo hii ni tafsiri kwamba ili kufanikisha hilo kwa ufasaha inaitajika rasilimali zingine kuwezesha mpango huo,” alisema Bi. Makala.