MGOMBEA URAIS CCM DK.SAMIA AWAHAKIKISHIA WANANCHI LINDI KUNUFAIKA NA MRADI GESI YA LNG

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Lindi.

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia amewaambia wananchi wa Mkoa wa Lindi kuwa mradi wa 

kuchakata Gesi Asilia (LNG)unaokwenda kuwanifaisha wananchi wote wakiwemo mkoa huo.

Dk.Samia ameyasema  leo Septemba 25,2025 mkoani Lindi mkoani Lindi alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi wa katika mkutano wa kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

Amesisitiza mradi huo ni tumaini la wana Lindi kwa sababu utazalisha ajira na kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja.”Mradi wa LNG uliopo Likong’o Mchinga ni tumaini lenu. 

“Huu ni mradi mkubwa wa Dola za Kimarekani Bilioni 40 ni mkubwa sana. Anayewekeza lazima awe na uhakika wa pesa yake itamzalishia kitu gani na sisi tuwe na uhakika tutapata nini, mradi huu na maliasili yetu.”

Amefafanua kwamba wamekuwa na mazungumzo kwa miaka miwili na wanakaribia kukubaliana.”Tupo hatua za mwisho tukikubaliana tutasaini mkataba. 

“Tunawaahidi mradi upo, lazima ilikuwa tuzungumze tuelewane tujue tunapata nini na wao wanapata nini tuelewane. Ndio maana Chuo cha Ufundi wa Umeme kitajengwa ili vijana wetu wapate ajira kwenye hilo eneo hilo.”

Pamoja na hayo Mgombea Urais Dk.Samia ameelezea mkakati wa Serikali ni kuifungua mikoa ya Kanda ya Kusini ikiwemo Lindi, Mtwara na Ruvuma.

“Katika Mkoa wa Lindi tutakuwa na Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Wilayanya Ruangwa. Vilevile ule utaratibu wa Chuo cha Veta kila mkoa hapa Lindi pia tutajenga,” amesema.

Wakati huo huo akizungumzia mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa, Dk. Samia ameeleza mradi huo utakaogharimu Sh.bilioni 279.5 na itazalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja takriban 30,000.

Pia Meli za uvuvi zitatia nanga kununua na kuleta samaki. Ndiyo maana kuna mradi wa kupeleka umeme mkoani humo ili kuwa na umeme wa uhakika kwa lengo la kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki kabla ya kuwauza.”Mradi wa Gridi imara utakaoanzia Ruvuma, Lindi na Mtwara kwa gharama ya Sh.bilooni  143.”

Awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimuaga Dk. Samia ambaye leo alihitimisha ziara yake ya kuomba kura Mkoa wa Lindi kwa kumhakikishia ushindi wa kishindo kwa kuwa kazi iliyofanyika inaonekana.

“Kila anapofika mgombea wetu wagombea ubunge wameeleza miradi iliyofanyika kwenye nchi yetu. Tuna sababu zote za Watanzania kumpigia kura Dk. Samia, pamoja na wabunge na madiwani ili muunganiko huu ulete umoja  na kuzitambua changamoto na kiziteleleza kwa wakati,” ameeleza Waziri Mkuu.