WASIRA AUNGANA NA DK. NCHIMBI , DK. MWINYI KATIKA MAZISHI YA ABBAS MWINYI

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Stephen Wasira ameungana na Mgombea mwenza wa Urais Dkt. Emmanuel Nchimbi na viongozi mbalimbali kushiriki mazishi ya Mtoto wa Rais Mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abbas Ali Mwinyi yaliyofanyika Bweleo Zanzibar.

Mbali na kushiriki mazishi hayo, Wasira alitoa pole kwa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali ambaye ni ndugu wa marehemu Abbas Mwinyi.

Abbas Mwinyi alifariki dunia jana mjini unguja, na maziko yake yamefanyika leo Bweleo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.