Watu wasioona kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani wamenufaika na mafunzoyaliyotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa lengo la kuwawezesha kushiriki shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia kanuni bora za usalamana afya kazini.
Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yametolewa kwa wanachama 50 wa Jumuiya yaWasioona Tanzania (TAB) yamehusisha mada mbalimbali zikiwemo utambuzi naudhibiti wa vihatarishi vya usalama na afya pamoja na misingi ya huduma ya kwanza mahali pa kazi. Washiriki wa mafunzo hayo wanajihusisha na shughuli mbalimbalizikiwemo ushonaji, kilimo, ufugaji, uzalishaji wa bidhaa zikiwemo sabuni na biasharandogondogo.
Akifungua mafunzo hayo, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesemaTaasisi anayoiongoza inatambua thamani na mchango wa watu wenye ulemavu katikakujenga uchumi wa Taifa jambo ambalo limepelekea mafunzo hayo kuandaliwa pamojana mafunzo mengine ambayo OSHA imekuwa ikayatoa kwa makundi mbalimbali yawatu wenye ulemavu.
“Niwapongeze washiriki wote wa mafunzo kwa kuitikia mwaliko wa kushiriki mafunzohaya muhimu kwenu kwani ni dhahiri kuwa ulemavu ni hali tu ambayo haipaswi kuwakikwazo kwenu kushiriki katika shughuli za kiuchumi,” amesema Mtendaji Mkuu waOSHA na kuongeza:
“Sambamba na mafunzo haya, tutawapatia vifaa saidizi zikiwemo fimbo nyeupe, karatasi za nukta nundu pamoja na vitabu maalum vya nukta nundu vyenye maudhui yamafunzo ya usalama na afya kwa ajili ya rejea zaidi.”
Aidha, Bi. Mwenda ameahidi kuwa mafunzo ya usalama na afya kwa makundimbalimbali ya watu wenye ulemavu yatafuatiwa na zoezi la kutembelea maeneo yao yakazi kwa ajili ya kutathmini mazingira ya kazi ili kushauri namna sahihi ya kuboreshamazingira hayo.
Awali, akiwasilisha salamu za Jumuiya ya Wasiiona Tanzania, Mwenyekiti wa Jumuiyahiyo, Bw. Omary Itambu, ameipongeza OSHA kwakuwa mstari wa mbele katikakuwawezesha watu wasioona pamoja na makundi mengine ya watu wenye ulemavu.
“Tunaiomba OSHA kuendeleza utamaduni huu wa kutujali watu wenye ulemavu. Kwa niaba ya washiriki wenzangu niwahakikishie OSHA kuwa mafunzo mliyotupatia si tuyatakwenda kuimarisha afya na usalama wetu bali yatatusaidia sana kuongeza thamaniya huduma na bidhaa tunazozalisha,” amesema Bw. Itambu.
Aidha, Bw. Itambu ametoa wito kwa washiriki wenzake wa mafunzo kuwa mabaloziwazuri wa OSHA ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wenzao ambao hawakupata fursaya kushiriki mafunzo.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wengine wa mafunzo, Mratibu wa Idara ya Vijana wa Jumuiya ya Wasioona, Bw. Bakari Hassan, amesema jambo lililofanywana OSHA ni la kuigwa na Taasisi nyingine za kiserikali na zisizo za kiserikali, akisisitizakwamba mafunzo hayo na vifaa saidizi walivyopewa vitarahisisha utendaji na kuongezatija katika shughuli zao za kila siku.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania (TAB), Bw. Omary Itambu, akiwasilishasalamu za TAB katika tukio la kufunga mafunzo ya usalama na afya mahali pa kaziyaliyotolewa na OSHA kwa wanachama wa Jumuiya hiyo wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Afisa Mafunzo wa OSHA, Bw. Simon Lwaho, akiwasilisha mada kuhusu vihatarishimahali pa kazi na udhibiti wake kwa wanachama wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania(TAB) katika semina ya mafunzo iliyoandaliwa na OSHA kwa kundi hilo.
Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza wa OSHA, Bi. Moteswa Meda akiwasilisha madakuhusu Misingi ya Huduma ya Kwanza mahali pa kazi kwa wanachama wa Jumuiya yaWasioona Tanzania (TAB) katika semina ya mafunzo iliyoandaliwa na OSHA kwa kundihilo.
Mtendaji Mkuu Wa OSHA Bi. Khadija Mwenda akikambidhi Mwenyekiti wa Jumuiya yaWasioona, Bw. Omary Itambu vifaa saidizi vikiwemo vitabu vya usalama na afya vyenyemaandishi ya nukta nundu, karatasi maalum za nukta nundu pamoja na fimbo nyeupekwa ajli ya wanachama wake.
Washiriki wa mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi ambao ni wanachama waJumuiya ya Wasioona Tanzania, wakifuatilia mada mbalimbali katika seminailiyoandaliwa na OSHA kwa ajili ya kundi hilo la watu wenye ulemavu.Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda pamoja na wakurugenzi na wakufunzi waOSHA wakifuatilia mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHAkwa wanachama wa Jumuiya ya Wasioona Tanzania Jijini Dar es Salaam.