Meridianbet Yawagusa Watu Wenye Ulemavu Wa Ngozi Kupitia Ugawaji Vifaa Kinga

IKIWA na dhamira ya kuleta mabadiliko chanya nje ya uwanja wa michezo, Meridianbet imefanya zoezi maalum la kugawa vifaa kinga kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Katika tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam, kampuni hiyo ilitoa kofia na miwani ya jua kwa walengwa, vifaa vilivyobuniwa mahsusi kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya mionzi hatari ya jua. Hatua hii inalenga kuimarisha afya na ustawi wa kundi hili maalum, ambalo mara nyingi hukumbwa na changamoto za kiafya kutokana na mazingira ya joto kali.
Mwakilishi wa Meridianbet wakati wa tukio hilo alisema “Tunapoangalia jamii, tunaona zaidi ya wateja, tunaona binadamu wenye ndoto, changamoto na matumaini. Kupitia msaada huu, tunaleta si tu kinga, bali pia tumaini na uthibitisho kwamba hawako peke yao.”
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi. Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Wanufaika wa msaada huo walipokea vifaa kwa furaha na shukrani, wakieleza kuwa msaada huo utawasaidia kuishi kwa ujasiri na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii bila hofu ya madhara ya jua.
Zoezi hili linaakisi falsafa ya Meridianbet ya “kujali zaidi ya biashara”, ambapo kampuni inawekeza katika miradi ya kijamii inayogusa maisha kutoka sekta ya afya, elimu hadi mazingira. Kwa kila hatua, Meridianbet inaendelea kuthibitisha kuwa uwajibikaji kwa jamii ni msingi wa utendaji wake.