Mechi za EPL, La Liga na Serie A Kukupa Mkwanja Wa Meridianbet – Global Publishers


Mashabiki na wapenzi wa soka kote duniani wanatarajia kupata burudani murua kushuhudia, miamba ya soka barani Ulaya wakipambana kusaka pointi muhimu. Na kwa wapenda kubashiri basi wanafurahi uwepo wa odds kubwa na machaguo mengi pale meridianbet.

Aston Villa wanacheza dhidi ya Fulham mchana wa leo. Villa wanatafuta ushindi wa kwanza msimu huu, huku Fulham wakijivunia safu ya kiungo. Mechi hii ni fursa kwa Villa kujitetea na kupata ushindi wa kwanza wa ligi. Odds kwenye mchezo huu ni kubwa kuhakikisha muwekezaji unavuna faida ya kutosha.

Saa 12:30 jioni tutawashuhudia Newcastle United dhidi ya Arsenal. Hii ndiyo mechi ya siku. Arsenal wanapambana kuendeleza kasi yao ya ushindi baada ya kutoa suluhu mechi yao ya mwisho dhidi ya City, lakini Newcastle wakiwa nyumbani wanaweza kugeuza meza. Kwa mashabiki wa kubashiri, hii ni mechi ya mabao na odds zake ni bomba sana.

Vilevile, kuna michezo mingine ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds kabambe. Kujiunga ni rahisi mno, tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#

Vilevile, ndani ya La Liga Rayo Vallecano anacheza na Sevilla mnamo saa 09:00 alasiri. Rayo Vallecano wanahitaji ushindi baada ya matokeo ya kusuasua kwani wameambulia ushindi mara moja pekee kwenye mechi tano za ligi tangu kuanza kwa msimu huu.

Elche nao wapo nyumbani kuwakaribisha Celta Vigo. Elche wakiwa nafasi ya tano wanacheza na timu inayoshika nafasi ya 15. Dimba la Estadio Martinez Valero halijawashuhudia Elche wakipoteza mchezo tangu kuanza kwa ligi hivyo Celta Vigo wana kibarua kizito kuondoa rekodi ya mwenyeji.

Mechi nyingine kubwa itakua pale dimbani Spotify Camp Nou, vijana wa Hansi Flick watakapowakaribisha Real Sociedad. Barcelona wanaingia uwanjani bila nyota wao Lamine Yamal. Sociedad hawajawa na matokeo mazuri msimu huu na wanaenda kukutana na mwiba mgumu sana hii leo.

Kwingineko ndani ya Serie A, AC Milan yupo nyumbani akiwakabili Napoli. San Siro inawaka moto hii leo Milan wanahitaji pointi tatu ili kujisogeza karibu na kilele cha msimamo lakini Antonio Conte na timu yake wakiwa vinara wa ligi hiyo hawajapoteza mchezo wowote ule kwenye michezo minne ya awali hivyo huu utakua ni mfupa mgumu mbele ya AC Milan. Hii ni mechi bora sana kwa kila mbashiri kuweka dau lake.

Stadio Olimpico Rome itawashuhudia wenyeji Roma wakikipiga dhidi ya Verona mapema kabisa saa kumi jioni. Roma ni moja ya timu zilizoanza kuonyesha dalili ya kuutaka ubingwa mapema huku Verona ikiwekwa kundi la timu zinazopambania kuwepo ligi kuu kwa msimu ujao. Hii mechi kwa odds ilizopewa pale Meridianbet, si ya kukosa kuwekea bashiri.

Jumapili ya leo ni ya kumaliza kiutajiri kwa kupata burudani ya soka safi la ulaya huku ukisubiri mechi zikamilike uweze kupokea faida ya ubashiri uliouweka na meridianbet kwani huku pesa ni uhakika.