Dk Mwinyi aahidi ujenzi wa masoko ya kisasa kuimarisha biashara Zanzibar

Unguja. Ili kuimarisha biashara na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa, mgombea urais wa Zan-zibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Mwinyi, ameahidi kuendelea na mpan-go wa kujenga masoko mapya ya kisasa ili ku-rahisisha upatikanaji wa bidhaa kisiwani Zanzi-bar.

Maeneo yanayotarajiwa kujengwa ni Mwera, Kisauni, Fuoni na Kwa Haji Tumbo, ili kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na kutoa mazingira bora ya kufanyia biashara.

Akizungumza leo, Jumatatu Septemba 29, 2025, wakati wa ziara yake katika Soko la Mwa-nakwerekwe, Dk Mwinyi amesema soko hilo tayari limekuwa dogo kutokana na wingi wa wafanyabiashara, hivyo kuna ulazima wa kupanua na kujenga masoko mengine ya kisasa.


“Tatizo la vibaraza litabaki historia tukiongeza masoko mapya. Niliahidi mitaji, na kwa kiwango kikubwa tumeweza kuwafikia. Tutaendelea kuongeza nguvu ili wafanyabiashara wote wapate maeneo mazuri ya kufanyia kazi zao kwa heshima na staha,” amesema Dk Mwinyi.

Dk Mwinyi pia amebainisha kuwa Serikali itaon-geza fungu la mikopo na kuweka utaratibu nafuu wa kodi ya Sh30,000 ili wafanyabiashara waimudu bila mzigo mkubwa.

Amesema pia kuwa katika kipindi kilichopita, Serikali ilitoa Sh96 bilioni kwa ajili ya mikopo ya kuimarisha mitaji ya wafanyabiashara, na ahadi hiyo itaendelezwa kwa nguvu zaidi.

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi akiwaonesha sehemu ya kutiki kumchagua siku ya kupiga kura Oktoba 29 wakati alipofanya ziara ya kutembea Soko la Mwanakwerekwe na kuzungumza na wafanyabiashara wa soko hilo ikiwa ni sehemu ya kampeni za chama hicho kusaka kura kuingia madarakani kwa kipindi cha pili



Ametumia fursa hiyo kuwasihi wafanyabiashara hao kuhakikisha wanaiunga mkono CCM katika uchaguzi mkuu ujao ili kuendeleza kasi ya maendeleo na kuwapa mikopo mikubwa zaidi.

“Kama mnataka uongozi unaoacha alama, basi tuendelee kushika madaraka. Tuliyoyaahidi mwaka 2020 tumetekeleza kwa vitendo, na mkiniweka tena madarakani, maendeleo yatakuja mara mbili zaidi.

“Nipigieni kura mimi kwa nafasi ya urais wa Zan-zibar, Samia Suluhu Hassan kwa urais wa Jam-huri ya Muungano, pamoja na wagombea wetu wa ubunge, uwakilishi na udiwani,” amesisitiza.

Kwa upande wao, wafanyabiashara wa soko hilo kupitia mwenyekiti wao, Nyundo Nyundo, wamemhakikishia Dk Mwinyi kuwa bado wana imani kubwa naye na watahakikisha kila mmoja anakuwa balozi wa mwenzake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29.

Hata hivyo, ameeleza changamoto zao, ikiwemo ukosefu wa mikopo, mzigo mkubwa wa kodi kutokana na mfumuko wa bei, pamoja na uche-leweshaji wa mizigo bandarini, ambao mara nyingi huwasababishia hasara.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Mohammed Said Dimwa, amewahimiza wafan-yabiashara hao kuendelea kumuunga mkono Dk Mwinyi na wagombea wa CCM, akiwakumbusha kuwa mwaka 2020 aliahidi kujenga masoko ya kisasa na utekelezaji wake tayari unaonekana kwa vitendo.