NIKWAMBIE MAMA: Rais ajaye anapaswa kujua haya
Kila rika huwa na mitindo yake ya maisha. Wakati fulani nilishuhudia wazee wetu wakivaa suruali pana na mashati ya kubana, wajomba na baba wadogo wakavaa mashati makubwa na suruali za kubana, sisi tuliokuwa wadogo tukavalishwa mitindo kwa kutegemea anayekuvalisha. Tuliweza kujuana kuwa huyu kavalishwa shati la “puto” na mjomba au “slim fit” na baba yake….