Andabwile afichua jambo Yanga | Mwanaspoti

Andabwile aliyewahi kutamba ndani ya Mbeya City na Singida Fountain Gate, kwa sasa anakipiga Yanga ukiwa ni msimu wake wa pili huku akianza vizuri 2025-2026 akiwa na uhakika wa namba kufuatia kuaminiwa na benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Romain Folz. Akizungumza jijini Mbeya wakati Yanga ikijiandaa kuikabili Mbeya City hapo kesho katika mechi ya…

Read More

Askofu Rugambwa azikwa Bukoba, huu hapa wasifu wake

Mwanza. Mwili wa Askofu Novatus Rugambwa umezikwa leo, Septemba 29, 2025, katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mama Mwenye Huruma, Bukoba mkoani Kagera. Hayati Rugambwa amezikwa jirani na Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa, Kardinali wa kwanza barani Afrika na aliyemrithisha jina lake pamoja na marehemu Askofu Nestor Timanywa, aliyemlea na kumpa daraja la upadri. Misa Takatifu…

Read More

Tuimarishe Lishe, Tupunguze Magonjwa Sugu

…………… NA. MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amewataka wadau kushirikiana na Serikali katika kuimarisha hali ya lishe nchini ili kupunguza kasi ya kuenea kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Amesema ulaji usio faa na mitindo mibaya ya maisha vimechangia kuongezeka kwa magonjwa…

Read More

Kesi ya kikatiba kupinga ulimaji, matumizi ya tumbaku Tanzania yatupwa

Dodoma. Mahakama Kuu imeitupa kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Watanzania wanne wakiibana Serikali isitishe kilimo na matumizi ya tumbaku, ikiwamo uvutaji wa sigara, kutokana na dosari za kisheria zilizobainika wakati wa kulipia nyaraka. Uamuzi wa kulitupa shauri hilo umetolewa Septemba 25, 2025, na nakala ya hukumu kupatikana leo Septemba 29. Katika kuhakikisha afya ya Watanzania…

Read More

Malindi yarejea Unguja na pointi tatu za Chipukizi

TIMU ya Malindi kutoka Unguja, imefanikiwa kuvuna alama tatu kwa kuifunga Chipukizi bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar iliyochezwa Septemba 27, 2025 kwenye Uwanja Gombani uliopo kisiwani Pemba. Bao hilo lilifungwa na Tchakei Moucheri dakika 15 akimalizia pasi ya Ramadhan Mponda ambapo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa…

Read More

Abood awajibu wakosoaji, aahidi maendeleo Morogoro Mjini

Morogoro. Mgombea ubunge  Morogoro Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdul-Aziz Abood, amewajibu wakosoaji wake wanaodai kuwa hajafanya kazi katika kipindi cha miaka 15 aliyokuwapo bungeni, akibainisha kuwa maendeleo yaliyopatikana jimboni humo ni ushahidi wa kazi zake. Abood ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 29, 2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Kata…

Read More

Watuhumiwa wa Mauaji ya Shyrose Mabula Wauawa na Polisi Mbeya – Video – Global Publishers

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, limetoa taarifa kuwa watuhumiwa watatu waliokuwa wakituhumiwa kumteka kisha kumuua Shyrose Mabula, mwanafunzi wa Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Mbeya, Shyrose Mahande (21), wameuawa wakati wakijaribu kupambana na polisi wakati wa ukamataji wao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, amewataja waliouawa kuwa ni Marwa Nyahega,…

Read More