Ligi Bara yambeba kipa Mkongomani
ALIYEKUWA kipa wa Dodoma Jiji, Mkongomani Alain Ngeleka, amesema Ligi Kuu Bara imempa fursa ya kuonekana zaidi baada ya nyota huyo kukamilisha uhamisho wa kujiunga na kikosi cha Bandari ya Kenya kwa ajili ya kukitumikia msimu wa 2025-2026. Akizungumza na Mwanaspoti, Ngeleka alisema kucheza kwa muda mrefu katika Ligi Kuu Bara kumechangia kupata nafasi hiyo…